October 25, 2015



Na Saleh Ally
Tayari nimejiandaa, naanza safari ya kwenda kupiga kura baada ya mazoezi yangu ya asubuhi.


Tafadhari Mtanzania mwenzangu, jindae nenda kapige kura kwa kuwa ni haki yako.

Husa sababu ya kuwa na hofu, iamini nchi yako kwamba ina uwezo wa kukulinda.

Tafadhari nenda kaitumie haki yako kumchagua kiongozi umpendaye.

Kila ufanyacho, kumbuka nchi yetu inahitaji amani na kuna maisha baada ya uchaguzi. Achana na kushawishiwa na wajinga wachache wenye nia ya kuona kuna vurugu kwa maslahi yao binafsi, usifanywe kuwa maslahi.

Wewe ni sehemu ya suala la utunzani amani hiyo. Fujo haitakusaidia lolote, pia usisahau tunatakiwa siku moja kuikabidhi nchi yetu salama kwa vizazi vijavyo na haiwezi kuwa salama kama hakuna amani.


Tanzania ndiyo nyumbani kwetu, mahali petu na hatuna pa kukimbilia. Achana na hisia za mihemko, kapige kura na itunze amani yetu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic