October 9, 2015

KOCHA WA TOTO AFRICAN, JOHN TEGETE AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE
Wachezaji wa Toto Africans wamegomea kufanya mzoezi kutokana na madai mbalimbali ya fedha wanayoidai klabuni hapo.


Habari za ndani ya klabu hiyo baada ya kufanyika ufuatiliaji zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji waIisema mgomo huo unatokana na madai ya fedha za usajili, mishahara, posho za safari na za michezo yao ya nje ya mkoa.

Alipoulizwa juu ya hilo, Makamu Mwenyekiti wa Toto, Waziri Gao, alisema: “Kweli wamegoma wakidai maslahi yao mbalimbali lakini uongozi unalifanyia kazi.”

Alisema kiasi ambacho wanachodai wachezaji hao kinafika shilingi milioni 12, alisema kuwa kama fedha hizo hazitapatikana basi huo ndiyo utakuwa mwisho wao kwa kuwa hawana njia nyingine ya kupata fedha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic