Chini ya Kocha Hans van der Pluijm, Yanga imeendelea na
mazoezi makali kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.
Licha ya idadi ndogo ya wachezaji kutokana na wengi kuwa
katika timu zao za taifa zinazoshiriki michuano ya Chalenji nchini Ethiopia,
mazoezi ya leo yaliendelea kuwa makini na hakuna utani.
Awali yalianza kama taratibu hivi, lakini baadaye ikawa ni
mbiobio.
Wakati walipojigawa, zikawa ni ushindani mkali utafikiri
mechi na kila upande ulionekana kupania kushinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment