Na Saleh Ally
Zanzibar Heroes imepoteza mechi zake zote mbili za michuano
ya Chalenji.
Imeanza kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Burundi, mechi ya pili
ikatandikwa tena kwa mabao 4-0 dhidi ya Uganda.
sasa inakutana na Kenya ikiwa ni mechi yake ya mwisho kama ya kujifurahisha vile.
Zanzibar Hereos, moja ya timu zilizokuwa hazitabiriki katika michuano ya Chalenji kwa maana ya ugumu. Imepoteza karibu kila mchezo.
Huenda linawezekana likaonekana ni kama jambo la kawaida tu,
lakini kuna mengi sana ya kuangalia katika soka la Zanzibar.
Timu hiyo kuchapwa mabao matano katika mechi mbili, kupoteza
mechi zote mbili bila ya kufunga hata bao moja, lazima tukubali kuna tatizo.
Zanzibar sasa si soka uwanjani, badala yake ni soka mdomoni kwa kuwa malumbano ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi badala ya soka la utendaji.
Soka la utndaji, watu wangekuwa wakijadili matokeo na uchezaji
bora. Lakini sasa kila mmoja anamshitaki mwingine mahakamani au anamlaumu
mwingine kwa kukosea.
Viongozi wa Zanzibar wana tatizo, lazima wajue malumbano yao
yanaufanya mchezo wa soka kuwa sawa na siasa na wanapaswa kulirekebisha jambo
hilo.
Hakuwezi kuwa na maendeleo kama mfumo wa sasa wa soka
Zanzibar ndiyo unaonekana ni chachu. Lakini kila mmoja akubali katika nafsi kwa
kulumbana kipuuzi ni kuuangamiza mchezo wa soka.
Zanzibar ina vipaji rundo hata sihitaji kutoa mifano. Lakini
vurugu, chuki na ubabaishaji wa viongozi wengi wa soka Zanzibar, kunazidi
kuiangamiza kisoka.
Najua baada ya muda, viongozi haohao ndiyo watakaokuwa
wakiinua mdomo kuanza kulaumu kwamba wamesahauliwa, au Zanzibar imesahauliwa. Lakini
wao ndiyo wanaoipotezea muda sasa kwa kulumbana tena kwa ajili ya matumbo yao.
Acheni ujinga, acheni kuua soka ya Zanzibar na kama
mmeshindwa ondokeni na muache Wazanzibar wengine wenye mapenzi ya dhati na
maendeleo yas oka, wafanye kazi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment