Uongozi wa Klabu ya Simba umeeleza kuwa unatarajia
kumleta mshambuliaji mpya kutoka katika timu za hapa Bongo kwa ajili ya kufanya
majaribio na iwapo atafuzu kocha Dylan Kerr atakuwa na jukumu la kumsajili.
Simba kwa sasa ipo katika mkakati mzito wa kufanya
marekebisho katika kikosi chake kufuatia upungufu uliyojitokeza katika nafasi
ya ushambuliaji kwenye michezo kadhaa ya ligi waliyocheza.
Mratibu wa Simba,
Abass Ally, amesema wanatarajia kumpokea mshambuliaji huyo ndani ya wiki hii
ili aanze majaribio.
“Kuna mchezaji anatarajia kutua ndani ya wiki hii kwa
ajili ya kumfanyia majaribio ambaye anatoka katika timu za hapahapa Tanzania, anacheza
nafasi ya ushambuliaji, hivyo kocha Kerr atakuwa na jukumu la kumuangalia uwezo
wake na kufanya maamuzi.
“Mchakato uliopo Simba ni kuhakikisha tunafanikiwa
kumaliza tatizo la ushambuliaji, hivyo iwapo mchezaji huyo ataonyesha uwezo
basi tutamsajili,” alisema Abbasi.
Wakati huohuo, kiongozi huyo amesema wanampango wa
kuwapeleka wachezaji watatu kwa mkopo ili waweze kusajili wengine.
“Kuna wachezaji watatu ambao wanatarajiwa kutolewa kwa
mkopo, lakini wawili kati yao ndiyo wenye uwezekano mkubwa wa kuondoka kwa kuwa
tayari tumeshawapatia timu.
“Lakini kuondoka kwao inategemea na makubaliano na
wachezaji wenyewe iwapo watakubali kutolewa kwa mkopo kwani jambo hilo
linahitaji maridhiano, lengo ni kuhakikisha tunafanikiwa kupata nafasi zaidi za
kusajili,” alisema Abbas.
0 COMMENTS:
Post a Comment