November 26, 2015


Kocha Mkuu wa Kili Stars, Abdallah Kibadeni amesema pamoja na kuwa wamepanga kushinda mechi zote za hatua ya makundi katika michuano ya Chalenji.


Kibadeni amesema pamoja na kuwa mchi ya mwisho ya makundi watamaliza na wenyeji Ethiopia, bado wanataka kushinda mchezo huo.

“Itakuwa mechi ngumu zaidi kwa kuwa tunakutana na wenyeji. Lakini lazima tushinde na tumepania kufanya hivyo.

“Kushinda mechi zote za makundi kuna faida mbili, kwanza kupata nafasi kwa uhakika hatua ya robo fainali.

“Pili imani ya kikosi kwa maana ya kujiamini kutokana na kushinda. Hali ambayo itasaidia katika mechi zijazo,” alisema.


Stars imecheza mechi mbili za michuano ya Chalenji ikianza kwa kuitwanga Somalia kwa mabao 4-0 kabla ya kivurumisha Rwanda kwa mabao 2-1 katika mechi ya pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic