Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic
amefanya kile alichowaahidi wakazi wa Malmo ambako ni mabao makuu ya klabu yake
ya kwanza.
Amieiongoza PSG kushinda kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya, lakini pia akafunga bao moja kama alivyoahidi.
Wakati alipotua Malmo, juzi aliwaambia mashabiki wa malmo
wamshangilie kama atafunga. Kweli amefanya hivyo katika dakika ya 49 lakini
alitengeneza mabao mengine mawili.
Alianza ndoto zake za mafanikio kisoka akiwa Malmo ambayo
baadaye ilimuuza Ajax ya nchini Uholanzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment