November 24, 2015


Kilimanjaro Stars inayonolewa na Abdallah Kibadeni imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuinyamazisha Rwanda kwa kuichapa kwa mabao 2-1.


Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Wassa, Stars ilipata bao moja katika kila kipindi.
Bao la kwanza lilifungwa na Said Ndemla na la pili likatupiwa na Simon Msuva katika kipindi cha pili baada ya kipa wa Rwanda kufanya uzembe.
Stars imefikisha ponti sita baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza.
Tayari ina nafasi ya kufuzu, kwani hata timu nyingine katika kundi lake itafikisha pointi 6, bado itakuwa na nafasi, zikifikisha timu mbili, bado itakuwa na nafasi ya best looser.

Mechi ya mwisho ya Kili Stars hatua ya makundi itakuwa dhidi ya wenyeji Ethiopia walioanza michuano kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rwanda.
Katika mechi ya awali, Zanzibar Heroes iliandikwa mabao 4-0 Uganda ambao walianza michuano hiyo kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Kenya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic