Kiungo mshambuliaji, Brian Majegwa amesema kamwe
hatajivunga kama akipata nafasi ya kucheza Simba.
Majegwa ambaye bado ana mgogoro na Azam FC, kwa mara
nyingine amesema angependa kumalizana na Azam FC ili aondoka.
“Mpira una mzunguko, sina maana nataka kugombana na
Azam FC. Ninataka kuondoka niende na maisha yangu,” alisema.
Alipoulizwa kama akipata nafasi ya kuitumikia Simba
ambayo sasa anafanya nayo mazoezi baada ya kuomba, akasema:
“Nafasi ya kuitumikia Simba, kwangu litakuwa jambo
bora kabisa. Nitafurahi na kufanya kazi hiyo kwa juhudi zote ili nifanikiwe.”
Taratibu suala la Majegwa linaanza kuchukua vichwa vya
habari katika vyombo mbalimbali vya habari kwa Azam FC imesema Mganda huyo bado
mali yake na ilimpeleka kwa mkopo KCCA ua Uganda.
Lakini Majegwa anasema hajalipwa mshahara wa miezi
mitatu hadi sasa. Hivyo angependa kupata haki yake, lakini pia apewe nafasi ya
kuondoka akiamini mkataba umeishavunjika.
Kuna taarifa nyingine kwamba Simba imeshamalizana naye,
lakini viongozi wake wamekuwa wakisisitiza, bado!
0 COMMENTS:
Post a Comment