PLUIJM AKIWA NA NGOMA. |
Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema Donald Ngoma ana uwezo wa kuwa
tishio zaidi ya sasa kama atazoea zaidi mikiki ya Ligi Kuu Bara.
Pluijm
raia wa Uholanzi amesema Mzimbabwe huyo ni mchezaji mwenye uchu na si mwoga.
“Anataka
kushinda, anapenda kupambana na anafurahia kufunga. Anaweza kuwa hatari zaidi
kama atazoea zaidi mazingira ya uchezaji wa ligi kuu.
“Unajua
kila anvyocheza mechi ndiyo anajifunza. Ninaamini atakuwa bora zaidi na kufanya
vizuri zaidi,” alisema Pluijm.
Ngoma
ni kati ya washambuliaji wenye kasi na uwezo mkubwa wa kumalizia.
Pia
mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea FC Platnums ya Zimbabwe ni kati
ya wachezaji hatari kwa mipira ya kichwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment