NJOHOLE AKIWA NA MKEWE.... |
Njohole aliyewahi kuwa nahodha wa Simba ambaye kwa sass anaendesha maisha yake nchini Uswiss, ameandika mtandaoni “I Stand in prayer with Burundi”. Akiwa na maana yuko upande wa wale wanaosali kwa ajili ya Burundi.
Machafuko yanaendelea ndani ya Burundi ambayo ni jirani ya Tanzania na kumekuwa na matatizo makubwa baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea muhula wa nne.
Tanzania imekuwa moja ya nchi zinazoathirika kwa kiasi kikubwa na vurugu hizo. Na kuonyesha mambo si mazuri, Njohole aliweka picha ya mshumaa unaowaka kizani na kutupia maneno hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment