December 30, 2015


Serikali imesema ipo bega kwa bega na mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwan Samatta kokote aendako.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemuambia Samatta leo mbele ya waandishi wa habari kwamba Serikali itamuunga mkono kokote aendako.


“Tuko na wewe pamoja kokote uendako, pia ninakupongeza kwa kuwa sehemu ya changamoto kwa wengine kutokana na mafanikio uliyofikia,” alisema Nape.

Samatta ameishakubaliana na klabu ya Genk ya Ubeligiji na sasa limebaki suala la Genk kumalizana na TP Mazembe ili Januari shughuli za uhamisho zifanyike.


Samatta alitembelea ofisi za Waziri Nape na kusema alifika hapo kwa ajili ya kupata baraka kabla ya kwenda kokote.

“Nimekuja kupata baraka, baraka za wazazi ni jambo muhimu sana kwa mtoto, ndiyo maana nipo hapa,” alisema Samatta ambaye alielezea kuhusiana na mkataba wa Genk.

“Suala la kusaini bado, ila makubaliano yote yako safi. Nasubiri wao wamalizane na TP Mazembe baada ya hapo mambo mengine yatafuatia,” alisema Samatta.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic