Beki wa kulia wa Simba, Hassani Kessy, amerejesha matumaini kwenye kikosi hicho baada ya kupona maumivu ya mgongo.
Kessy alipata majeraha hayo kwenye Ligi Kuu Bara kabla ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea katika Visiwa vya Unguja, Zenji.
Kutokana na majeraha hayo, beki huyo ameshindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Muingereza, Dylan Kerr huku akiiacha nafasi yake ikichezwa na Mrundi, Emily Nimubona.
Kessy amesema kuwa leo Jumatatu anatarajiwa kuanza mazoezi ya gym kwa ajili ya kujiweka fiti.
Kessy alisema, hiyo ndiyo program atakayoanza nayo huku akikisubiria kikosi hicho kikirejea Dar kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.
“Ninashukuru ninaendelea vizuri hivi sasa, hiyo ni baada ya kupata matibabu mazuri kutoka kwa daktari wangu,” alisema Kessy.
0 COMMENTS:
Post a Comment