Bao la Mtibwa Sugar walilofunga katika 10 za mwisho za mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar katika michuano ya Mapinduzi, ndiyo gumzo zaidi katika mitandao leo.
Bao Hilo lilifungwa na Ramadhani Kichuya na mwamuzi msaidizi akainua kibendera kuonyesha mfungaji kabla aliotea, ingawa mazingira yote yalipingana na mwamuzi huyo.
Kutokana na hali hiyo, mashabiki wa soka wamekuwa wakilijadili bao hilo, wengi wakionekana kupinga kwamba kuna walakini lakini wako wanaoamini mwamuzi alikuwa sahihi.
Mjadala umekuwa mpana zaidi katika makundi mengi ya wapenda soka, wakibishana na kujadiliana kwamba kipi ni sahihi au si sahihi.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1 huku Mtibwa Sugar ikionyesha soka safi na la kuvutia ingawa ilishindwa kuibuka na ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment