Mbwana Samatta sasa rasmi amesaini Genk ya Ubelgiji na kukabidhiwa jezi namba 77.
Lakini haikuwa kazi rahisi kwani pamoja na Wazungu kumkubali uwanjani, lakini alilazimika kutimua mbio tena kasi kubwa ili kupima afya yake.
Hiyo ilikuwa ni kutaka kujua uhakika wa viungo vyake au kwa kifupi vipimo vya afya.
Kwa sasa Samatta ni mali ya Genk ambayo imeingia naye mkataba wa miaka minne utakaoisha mwaka 2020.










0 COMMENTS:
Post a Comment