January 29, 2016


Mbwana Samatta sasa rasmi amesaini Genk ya Ubelgiji na kukabidhiwa jezi namba 77.

Samatta amekabidhiwa jezi hiyo leo mchana katika hafla fupi ya kumambulisha mbele ya waandishi wa habari kwenye mji wa Genk.

Amejiunga akitokea TP Mazembe kwa mkataba wa miaka minne na nusu, mkataba wake unamalizika mwaka 2020.


Samatta sasa atakuwa akivaa jezi za rangi ya bluu za KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Kwa sasa ndiye nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars. Kabla ya kwenda Ulaya ameichezea Stars mechi 20 na kufunga mabao 7.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic