January 4, 2016


Wakati kikosi cha Azam FC kikimkosa beki wake Aggrey Morris, kocha mkuu wa timu hiyo Stewart Hall, amefunguka kuwa sasa beki wake kisiki Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ameshuka kiwango na limebaki jina tu.

Hall raia wa Uingereza alisema licha ya kumkosa Morris lakini kiwango cha Wawa kwa sasa kimeshuka zaidi kutokana na kucheza muda mrefu.

“Kiukweli Wawa kwa sasa hayupo vizuri kama alivyokuwa msimu uliopita kutokana na kucheza mechi nyingi bila kumpumzika, lakini nalazimika kumtumia kwa kuwa sina mchezaji mwingine bora kwa sasa .

“Kucheza anacheza lakini siyo kwenye kiwango kikubwa cha kutisha ila kwa kuwa ni mzoefu uwanjani na ukubwa wa jina lake nadhani amekuwa ni msaada kwenye timu hii,” alisema Hall.


Katika mechi ya jana ya Kombe la Mapinduzi, Hall alimpumzisha Wawa katika kikosi chake kilichoivaa Mtibwa Sugar na kupata sare ya bao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic