FURAHA ya Wanasimba wengi ilikuwa ni kuibuka na ushinda wa bao 1-0 dhidi ya kikosi cha Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara katika mechi pekee ya ligi hiyo iliyochezwa wikiendi.
Kwanza nianze na kulaani vitendo vya kijinga ambavyo mashabiki wa Ndanda waliingia kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona ambako Simba walikuwa wakifanya mazoezi na kufanya vurugu.
Kama haitoshi, waliwasubiri wakati wanatoka na kuwapiga mapewe jambo linaonyesha kiasi gani watu kadhaa wasivyo na uelewa, wasivyo wanadamu na wasiojua thamani ya utu.
Vizuri Ndanda FC wasitengeneze kichaka cha wapuuzi kama hao, TFF inapaswa kulaani na Jeshi la Polisi Tanzania linapaswa kuwafikisha mahakamani hao waliokuwa wakifanya upuuzi huo ili wachukuliwe hatua na iwe mfano kwa wengine kwamba soka si matusi, ugomvi au kulenga kuumizana.
Nikirejea katika mechi hiyo kama nilivyoanza, siku hiyo Kocha wa Simba, Dylan Kerr aliweka rekodi ya aina yake alipoamua kupanga kikosi cha kwanza chenye wachezaji saba wa kigeni.
Kawaida TFF inaruhusu wachezaji saba wa kigeni, hivyo Simba iliwatumia wote katika mechi moja. Mechi ikaisha timu hiyo kuibuka kwa ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa ni mzalendo, Ibrahim Ajib ‘Cadabra’.
Najua furaha ya Wanasimba ilikuwa ni huo ushindi wa bao 1-0 ambao walikuwa wakiusubiri kwa hamu baada ya sare mfululizo mara baada ya ligi iliyokuwa imesimama kuanza tena.
Lakini hakuna aliyefikiria suala la wachezaji wa kizalendo kwamba kama hilo la Kerr kupanga wachezaji wote wa kigeni saba litaendelea, pia ni hatari kwa soka la Watanzania hapo baadaye.
Tunawahitaji wageni kama sehemu ya changamoto, ligi yetu ndiyo inakua, wachezaji wetu ndiyo wanainuka, hivyo wanahitaji nafasi ya kucheza. Kweli wanaweza kupambana na wageni lakini pia tukumbuke wanaweza kuangushwa na wageni pia.
Sijaandika makala haya kumlaumu Kerr, kwa kuwa amefanya hivyo mara moja tu. Lakini nimewahi ili kumkumbusha kwamba wageni ni sahihi lakini Watanzania wanataka maendeleo ya vijana wao hivyo ni vema wakapata nafasi.
Kama ambavyo amewapa nafasi hao wageni, basi vizuri aweze kuwapa nafasi vijana wa Kitanzania ambao wengi wana vipaji lakini wanahitaji mafunzo na morali kwa kocha wa nje kama yeye ambaye ndiyo itakuwa ni kazi yake.
Kerr anatokea Uingereza, kwa Tanzania naye ni mgeni, huenda anaweza akaangalia ushindi wa mechi yake moja au mbili bila kujali soka la Simba na Tanzania kwa ujumla pamoja na wachezaji wazawa ataliachaje. Chonde Kerr, vijana wetu wanahitaji kukua.
Tanzania inahitaji Watanzania kuiwakilisha. Kumbumbusha Kerr kuwa aendelee kuwapa nafasi zaidi wazawa, ninaamini itachangia wao kuendelea kujiamini na kutaka kufanya vizuri zaidi. Lakini pia nasisitiza suala la wao kuendelea kujituma ili kupata nafasi.
Maana yangu hivi, Kerr atoe nafasi kwa wazawa ili waonyeshe uwezo wao, lakini wakipata nafasi nao wafanye kweli, waachane na mambo ya kulalamika hovyo na kuwa na hadithi nyingi zisizokuwa na msingi hata kidogo.
Katika hili, pia ninaendelea kuweka msisitizo, TFF inapaswa kuliangalia upya suala la wachezaji wa kigeni hasa nafasi ya kipa. Sidhani kama ni sahihi kutegemea mlinda mlango kutoka nje ya Tanzania.
Kipaji cha Peter Manyika ambaye ni kinda na ana uwezo sasa kinakufa huku mkongwe kutoka Ivory Coast akiendelea kudaka. Miaka nenda rudi, Simba imeng’ara na makipa kutoka hapa nyumbani.
Hakika sikubali, ninapinga na ninaona ni uoga na usahihi uliopitwa na wakati Watanzania kutumia kipa wa kigeni wakati tuna vipaji na makipa kibao hapa nchini ambao hawana nafasi ya pa kuonyeshea uwezo wao. Si sahihi hata kidogo.
Lakin Ni vema kutumia technical zozoTe pale timu inapohitaj ushindi..kama mzawa hakun anayejituma atumie wagen tu..hizo ndo changamoto ili wajitume said
ReplyDeleteNo point here issue ya wageni saba nafikiri kocha as to base on players available based on training performance hapa kocha hana chakulaumiwa issue ya golie mgeni if your are a true soka fan simba not a first club having foreign keeper mbona yanga imeleta hadi wazungu u never being against stop cheap football politics .
ReplyDeleteTatizo waandishi hamjui mnataka nini!! Puljim alipokuwa anamwanzishia benchi Bosou na Coutinho kwa kuwa watz wana kiwango kizuri mlipiga kelele na kukosoa uongozi wa Yanga kwanini asijiliwe mchzaji wa kimataifa anayekaa benchi!! Lakini mkasahau alikuwa analinda vipaji vya akina Mwaishuya, Cannavaro nk. Leo Kerr kafanya kweli bado mnalaumu, sasa nyie mnataka nini!? Mvua na Jua kwa wakati mmoja!? U can't be serious
ReplyDeleteWewe saleh unaanza taratiiiiibu kunifukuza kwenye blog ya kama kungekua na acount ungweza kujua naingia mara ngapi kwa siku. Na nazungumza hivi baada ya kumuona mchambuzi anakuwa na mawazo mgando kama hayo. Ni nini maana ya wachezaji 7 wa kigeni wasajiliwe kwa kilabu inayoweza kusaji. TP Mazembe huwa inachezesha mpaka wageni 10 na bado timu ya congo kila mwaka inashiriki mataifa huru barani afrika. Tumia akili afu amka kaka. Mlilalamika ooh wachezaji wa kigeni wapunguzwe kutoka wa5 hadi wa3 kwa kuwa wengine wanaozea benchi ooh fedha nyingi zinapotea leo wamepangwa wote mnalaumu tena. Duh! Mpewe nini ili mridhike
ReplyDeleteKweli umekupuka lakini umeonesha jinsi waandishi we2 mnavyoandika habari za kishabiki, kocha anaangalia jinsi wachezaji wanavyo training na kupanga kulingana na mahitaji yake, wachezaji wajitume Ili wapate nafasi first 11 hakuna zaidi ya Hilo.
ReplyDeleteha ha wala huitajo kuwa na kocha kujua kuwa agban is much better dan peter,,kajiachia kanenepa ,,mchezaji apewe nafasi kutokana na anavyo jituma na kuonesha mazoezin na sio kisa ni mtanzania
ReplyDelete