Kocha Jackson Mayanja ameonyesha hataki mchezo na kazi baada ya kumzuia mkongwe Mussa Hassan Mgosi kufanya mazoezi.
Pamoja na kumzuia Mgosi, Mayanja alimpa adhabu kiungo Said Ndemla akimbie kuzunguka uwanja.
Wote wawili walipewa adhabu hizo kutokana na kuchelewa kuwasili kwenye mazoezi kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam, jana. anaonekana hajaridhika.
Mgosi, alichelewa zaidi na Mayanja hakukubaliana na hali hiyo na kuamua kutoa adhabu hiyo, iwe fundisho kwake.
Tena adhabu ilikuwa kubwa zaidi kwa Mgosi kwa kuwa yeye ni mkongwe, hivyo anapaswa kuwa mfano bila ya kujali anaishi upande gani wa jiji la Dar es Salaam.
Unadhani baadaye Mayanja alimruhusu Mgosi kufanya mazoezi hata kidogo? Unajidanganya, alisugua benchi hadi mwisho akiwa mtazamaji.








0 COMMENTS:
Post a Comment