January 28, 2016

NDEMLA AKISHANGILIA BAO ALILOFUNGA DHIDI YA BURKINA FASO KATIKA MECHI YA KOMBE LA FA MJINI MOROGORO, WIKI ILIYOPITA.


Na Saleh Ally
Said Ndemla ni moja ya vijana wenye vipaji vya juu kabisa ambaye Tanzania imebahatika kuwa naye. Sasa anakipiga katika kikosi cha Simba.

Ndemla ni kijana ambaye hana makeke, anajitambua na hakika amekuwa akijituma kuhakikisha anafanya vizuri.

Utaona mara nyingi akiingia au kuanza katika kikosi cha kwanza cha Simba ay Taifa Stars, kumekuwa na mabadiliko fulani.

Amekuwa na tatizo dogo sana, nalo ni ule “utoto wa kimpira”, kufanya mambo ambayo kawaida huwakasirisha wale ambao wamelenga kitu fulani wakiwa siriaz.

Lakini ana kitu ambacho wengi hawana, “kujaribu lisilowezekana”. Mara nyingi anapenda kufanya vitu vipya, anajaribu kupiga mashuti ya kushitukiza, anataka kufunga akiwa katika sehemu inayoaminika haiwezi kufanikiwa.

Ndemla anataka kutoa pasi ambayo mwingine angehofia kutofanya hivyo. Kwa kifupi si mwoga wa lawama na hii itamsaidia sana kufanikiwa kama ataendelea kufanya hivyo kwa juhudi.

Mtu anayejaribu, mara nyingi huwaudhi wengine, iwe mashabiki, wachezaji wenzake au kocha. Lakini siku akiwafurahisha, inakuwa ni furaha isiyosahaulika.

Ndemla ana uwezo mzuri wa kufunga, uwezo wa juu wa pasi bora, anaweza kubuni mambo uwanjani. Pia hadi sasa ni kijana mwenye nidhamu, jambo linalowashinda wengi.

Kikubwa ambacho kinatakiwa ni kwa Ndemla kuendelea kuwa ni mtu asiyeridhika mapema au asiyefurahia kichache anachokipata.

Lakini Simba, lazima waamini umri wake wa ujana, kupotea pia ni rahisi. Lazima wawe karibu naye kwa kuwa hajafikia umri wa “aachwe aende mwenyewe”.


Mimi ninaamini Ndemla ni hazina, ambayo ikitunzwa na kujitunza itakuwa mbereko ya Tanzania kupitia kizazi tulichonacho na miama minne baadaye, ndiye atakuwa tegemeo au kiongozi wa Simba au timu nyingine atakayokuwa akichezea pia Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic