Unaweza kusema ilikuwa moja ya mechi ya upinzani kweli, lakini mwisho ni Azam FC imepata bao moja na wapinzani wao wakubwa Yanga bao moja.
mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi hatua ya makundi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo. ilikuwa na ushidani wa juu huku ikitawaliwa na ubabe wa hapa na pale.
Azam FC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 56 baada ya mabeki wa Yanga kujipanga vibaya na mfungaji akavunja mtego na kuuwahi mpira kabla ya kupiga shuti kali lililomzidi Deo Munishi ‘Dida’.
Yanga nao waliendelea kupambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 82 kupitia kwa Vicent Bossou baada ya krosi nzuri ya Msuva na mabeki Azam kutumia nguvu zaidi kumbana Donaldo Ngoma baada ya makosa ya kipa Aishi Manula ambaye alidaka mpira na kuudondosha.
Bao la Yanga lilipatikana dakika chache baada ya nahodha wa Azam FC, John Bocco kulambwa kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekundu.
Kila timu imecheza mechi ya pili, Azam FC ikifikisha pointi mbili baada ya sare ya kwanza ya mabao 2-2 dhidi ya Mtobwa Sugar, huku Yanga ikifikisha pointi 4 baada ya kuanza michuano hiyo kwa ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment