Kikosi cha Azam FC kitamaliza ziara yake nchini Zambia keshokutwa Jumatano kwa kucheza fainali ya michuano maalum dhidi aya Zesco.
Lakini uongozi wa Azam FC umetuma shukurani kwa mashabiki wake na uongozi wa TFF kwa kuwapa ruhusa ya kushiriki michuano hiyo maalum.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema wanatarajia kufanya vizuri katika fainali itakayokuwa ngumu.
“Lakini tunapenda tuwashukuru mashabiki wetu wanaotuunga mkono kwa muda wote katika ziara hii, wakiwa hapa Zambia na nyumbani.
“Lakini tuwashukuru TFF ambao walituelewa kuhusiana na ziara hii, imekuwa na manufaa kwetu, tunaamini kwa soka ya Azam FC na Tanzania kwa ujumla,” alisema Kawemba.
Azam itarejea nyumbani na kucheza viporo kwa kuwa timu nyingine zimekuwa zikiendelea na mechi za Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment