February 1, 2016


Winga hatari wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila amesema mshambuliaji Hamisi Kiiza wa Simba, ataendelea kusumbua kwenye Ligi Kuu Bara.

Tayari Kiiza amefunga mabao 12 baada ya kuichezea Simba mechi 14 za Ligi Kuu Bara. Simba imecheza mechi 12, yeye alikosa mbili.
Lunyamila amesema, Kiiza ana uwezo mkubwa sana wa kufunga na tayari ameizoea zaidi ligi kuu.


“Leo anacheza zaidi ya msimu wa tatu, si mgeni na ana uwezo wa kufanya vizuri zaidi. Ninaamini atasumbua sana kama hataumia hadi mwisho wa ligi,” alisema Lunyamila ambaye pia aliwahi kukipiga Simba na baaday Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic