March 23, 2016

Beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam, ambaye alizifunga Yanga na Azam kwenye Ligi Kuu Bara na kuipa timu yake pointi tatu katika michezo hiyo msimu huu, amesema mara baada ya msimu huu kumalizika, anatamani kurejea katika klabu yake ya zamani ya Simba.

Miraji ambaye yupo Coastal kwa mkopo akitokea Simba, mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu na amesema ataangalia ustaarabu wa wapi aende lakini nafasi ya kwanza ameipa Simba. Beki huyo alizifunga timu hizo katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga wakati Yanga ilipopoteza kwa mabao 2-0 huku Azam ikibamizwa bao 1-0.

MIRAJI
Beki huyo ameliambia Championi Jumatano kuwa, tangu atue Coastal kiwango chake kimekuwa kikiimarika siku hadi siku na kuamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Simba kumrejesha tena licha ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.

“Bado sijajua nitajiunga na timu gani baada ya msimu huu kumalizika kwani mkataba wangu utakuwa unamalizika, bado sijafikiria kubaki hapa Coastal, lakini kama mambo yakienda sawa, lolote linaweza kutokea.


“Lakini bado nataka kucheza Simba kwa mara nyingine tena, ninapokuwa uwanjani nafasi yangu hasa ni beki wa kati lakini zamani Simba mara kwa mara nilikuwa nikilazimika kucheza pembeni kutokana na mwenye namba hiyo kuwa majeruhi kwa muda mrefu,” alisema beki huyo.

Source: Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic