March 23, 2016


Pamoja na Danny Lyanga na Hamis Kiiza wa Simba kuendeleza moto wa kutupia kwenye Ligi Kuu Bara, lakini imebainika kuwa safu yao ya ushambuliaji ipo nyuma dhidi ya safu ya wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, inayoundwa na Simon Msuva, Amissi Tambwe na Donald Ngoma (MTN).

Safu ya Simba inayokamilishwa na Ibrahim Ajibu na kuunda AKL, imekuwa moto wa kuotea mbali baada ya kushinda mechi nne mfululizo na kuendelea kung’ang’ania kileleni mwa ligi hiyo lakini kimahesabu bado ipo nyuma dhidi ya wapinzani wao hao.

Mpaka sasa MTN, imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 36, Tambwe akifunga 17, Ngoma 13 na Msuva sita, huku AKL ikiwa imefunga 33 baada ya Kiiza kufunga mara 19 akiwa kileleni mwa wafungaji bora wa ligi, Ajibu akitupia tisa na Lyanga matano.

Hata hivyo, bado MTN inaonekana ni bora zaidi hata kwa mahesabu ya mechi walizocheza. AKL imefanikiwa kufunga mabao hayo 33 katika mechi zao 24 za Ligi Kuu Bara, huku MTN yenyewe ikifanikisha idadi ya mabao yao 36 kwa mechi 21 tu.

Bado MTN imeendelea kutamba na kuwa tishio hata kwenye baadhi ya timu za ligi hiyo ambapo mabao yao 36, yamezidiwa bao moja tu na mabao 37 yaliyofungwa na timu nzima ya Azam inayoshikilia nafasi ya tatu kwenye ligi ikiwa nyuma ya Yanga na Simba.

LYANGA

Mgambo JKT yenyewe inayoshikilia nafasi ya 12 imefunga mabao 20 tu ambayo ni nusu ya mabao ya MTN, licha ya kucheza mechi 23 mpaka sasa.

MTN imeisaidia timu yake kufikisha mabao 51 ya kufunga ikiwa ni mengi zaidi ya timu zote za ligi huku AKL ikiisaidia timu yao kuwa na mabao 43, mpaka sasa na kuwa timu ya pili iliyofunga mabao mengi zaidi.


Hata kwenye listi ya tano bora ya wafungaji bado MTN imekaa vizuri, imetoa wafungaji wawili kwenye listi hiyo. Anaanza Kiiza aliyefunga 19 kisha Tambwe mwenye 17, Ngoma 13 kisha Jeremiah Juma wa Prisons mwenye 11 na Elias Maguri wa Stand United aliyefunga 10.

1 COMMENTS:

  1. mimi nisingependa waitwe AKL, JINA LINALOWAFAA NI LAKI- unapolitamka linamaanisha bahati au 100,000

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic