March 24, 2016

SALEH ALLY "JEMBE" AKIWA NA MAREHEMU CRUYFF 

Huyu ndiye baba wa soka la kisasa, Johan Cruyff amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68.

Cruyff amefariki huku Tanzania ikiwa ndiyo nchi yake ya mwisho kuitembelea barani Afrika alipokuja mwaka jana na kikosi cha wakongwe wa Barcelona.

Gwiji huyo wa Ajax, Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa.

AKIWA NAHODHA BARCELONA

Wakati timu ya wakongwe ya Barcelona ilipokuja hapa nchini, niliona watu wengi walikuwa wkaipambana kuwavikia nyota kadhaa kama Patrick Kluivert na wenzake.

Kwangu akili niliielekeza zaidi kwa Johan Cruyff, nilijua ndiye gwiji kuliko wote na mchezaji mwenye rekodi za juu kabisa kupita wote waliokuwepo.

Alitwaa karibu kila kitu akiwa mchezaji na baadaye kocha. Alikuwa na tuzo rundo, hizi hapa baadhi; Alikuwa mchezaji bora wa dunia mara tatu 1971, 1973 na 1974. Alitwaa taji la ufungaji bora Kombe la dunia mwaka 1974 pia alikuwa kocha bora duniani mwaka 1987.

Nilitamani kuzungumza naye kutokana na kazi yake enzi hasa akiwa Barcelona. Lakini Kocha wa zamani wa Yanga, Ernie Brandts aliwahi kusema: “Uholanzi kuna rundo la vipaji vya soka, lakini hadi sasa hakuna mchezaji nyota na mwenye uwezo wa juu aliyewahi kutokea mfano wa Cryuff.”


FEGI NAZO ZILICHANGIA

Nilipokutana naye, alionekana ni mtu mchangamfu, nikamueleza ninahitaji kufanya naye mahojiano kwa muda naye.

Huku akiwahimiza wachezaji watoke kwenda uwanjani, Cruyff alisema: “Ntakuwa na kipya kweli. Muda kidogo umebana, tunaweza kuzungumza baadaye.”

Nikamuuliza vipi hakuwa amevaa jezi ili aonyeshe mambo ya enzi zake. Akajibu: “Sina lolote tena, nimekuwa mgonjwa mara kwa mara, kansa inanitafuna na hakuna hata matumaini.”


AKIITUMIKIA UHOLANZI DHIDI YA ARGENTINA...

Nikajaribu kumpa matumaini kwa kumwambia: “Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu.”
Akajibu kwa kuonyesha ishara ya kutoa macho na kubana mashavu huku akisambaza mikono yake. Tukapiga picha, nikamuacha aendelee na ratiba zake kwa wakati huo.


PUMZIKA KWA AMANI GWIJI.

1 COMMENTS:

  1. Salehjembe wakati ukiwa hodari wa kuona makosa ya Malinzi nawe pia ujue Blog yako ni kubwa, makosa ya kiuandishi hayaepukiki Johan Cruyff amefariki akiwa na umri wa miaka sitini na minane (68) na sio miaka nane (8) kama ulivyo andika. Najua ni haraka ya kutaka ku post hii habari.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV