NYONI (CHINI)...
Unaweza kusema ni sehemu ya pigo, hata kama ni dogo. Azam FC itamkosa beki wake, Erasto Nyoni katika mechi dhidi ya Yanga, Jumapili.
Yanga itaivaa Azam FC katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizoifikia blogu ya wanamichezo ya SALEHJEMBE zimebainisha kwamba Nyoni ana kadi tatu za njano.
“Nyoni tayari ana kadi tatu, Azam kama hawajui watajichanganya kwa kuwa alipewa kadi ya njano walipocheza na Prisons kule mbeya,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Juhudi za kuupata uongozi wa Azam FC zilifanikiwa leo mchana baada ya Msemaji wao, Jaffar Iddi ‘Mbunifu’ kutoa ushirikiano.
“Nina taarifa hizo, lakini nikuhakikishie Azam FC ni timu inayofanya mambo yake kiweledi na umakini mkubwa. Mchezaji hawezi kuchezeshwa akiwa na kadi tatu.
“Tuna rekodi za kila mchezaji na benchi la ufundi liko makini sana,” alisema Iddi.
Tayari joto la mechi hiyo linazidi kupanda kwa kasi kubwa huku mashabiki wakitaka siku ifike haraka, ubishi uishe.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment