March 1, 2016



Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuwasili leo mjini Dar es Salaam, tayari kwa maandalizi ya mwisho dhidi ya Yanga, Jumapili.

Azam FC ilikuwa mjini Moshi ambako ilikwenda kuivaa Panone katika mechi ya Kombe la Shirikisho linalodhaminiwa na Azam Sports HD.

Taarifa zinaeleza kikosi hicho kitawasili leo saa sita mchana kwa ndege kikotokea Arusha ambako kilikwenda baada ya mechi yao dhidi ya Panone.

"Tumeambiwa baada ya kufika Dar, wachezaji moja kwa moja watakwenda kambini. Hawataruhusiwa kwenda majumbani," kilieleza chanzo.

Wapinzani wao Yanga, tayari wapo kambini mjini Pemba wakijiandaa na mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wapenda soka nchini.

Yanga ipo katika nafasi ya kwanza, yaani ndiyo vinara wa Ligi Kuu bara wakiwa na pointi 46 sawa na Azam FC mwenye 46 ikiwa katika nafasi ya pili.

Atakayeshinda mechi hiyo, ndiye atakayekaa kileleni. Kama itakuwa sare basi Yanga ndiyo itaendelea kukaa kileleni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic