March 15, 2016


Bao la kwanza alilofunga beki wa Yanga, Juma Abdul wakati timu yake ilipocheza na Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Kigali, Rwanda limeendelea kuwa gumzo.

Bao hilo limekuwa gumzo katika jiji la Kigali, wengi wakijadili kuhusiana na ubora wa bao na kazi ya kipa wa APR.

Beki huyo alifunga bao hilo kutoka takribani mita 25 na shuti lake likajaa wavuni moja kwa moja.

Wako ambao wamekuwa wakisema kipa alikuwa mzembe kwa kuwa mpira huo wa adhabu ulipigwa kutokea mbali sana.

Lakini wengine wanaamini mpigaji alifanya kazi yake kwa kiwango cha juu, hivyo kipa yoyote hata angekuwa David De Gea wa Man United, angechemsha.


Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda kwa mabao 2-1, akianza kufunga Juma Abdul kabla ya Thabani Kamusoko kumaliza kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic