March 15, 2016

AMAHORO


Na Saleh Ally
Kwa wale waliobahatika kufika kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali pia katika Uwanja wa Taifa katika jiji kubwa la Dar es Salaam, wanaweza wakanielewa kwa urahisi zaidi, nini nitauliza pia ninataka kuelezea.

Uwanja wa Taifa, mali ya Watanzania ndiyo uwanja bora kabisa kuliko yote Afrika Mashariki na Kati. Una uwezo wa kuingiza uwanjani watu takribani 60,000 waliokaa vitini.

TAIFA

Kilichonifanya nihoji ni ubao wa matangazo, ingawa mara kadhaa nimekuwa nikifika kwenye Uwanja wa Amahoro ambao ni wa kizamani na hadi sasa, ni watu wachache wanaokaa vitini na sehemu kubwa wanakaa kwenye simenti au zege, lakini una ubao bora kabisa.

Ubao huo unaonekana ni bora kwa kuwa una mambo muhimu ikiwemo muda wakati mechi ikichezwa, muda wa mechi yenyewe na wakati mwingine hata hali ya hewa ya wakati husika.

Lakini ule ubao wa matangazo ndani ya Uwanja wa Taifa, unaonekana utafikiri ni wa miaka ya 1990. Hauna vitu vyote hivyo na muonekano wake hautoi picha bora kama huo wa Amahoro.

Uwanja uliojengwa zamani, unaonekana kuwa na kifaa bora kuliko uliojengwa hivi karibuni na ambao ni wa kisasa zaidi.

Ninachohoji, ule ubao ulio kwenye Uwanja wa Taifa “tumepigwa”? Au watu hawajui jinsi ya kuutumia, au wanajua lakini huwa wanapuuzia kwa kuwa Watanzania si watu wa kujali sana?


Bado muonekano wake si mzuri, ninamaanisha picha. Lakini bado nasisitiza hata mpangilio wa screen yenyewe kuonyesha mambo muhimu hauonyeshi. Tatizo ni nini hasa? Kama kuna anayejua tunaweza kushea na kujifunza zaidi. Karibuni tafadhari.

1 COMMENTS:

  1. Ule ubao cha sio kama technology yake ni ya kizamani tatizo ni vile vitu viko chini ya wachina... Na hata user interface ya lile screen ni ya kichina, sasa kuto kujali kwetu kuna pelekea vitu vya muhimu vya kupasha taarifa havifikii watazamaji kama inavyo takiwa... Meneja wa uwanja ni tatizo pale

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV