Nahodha wa Simba, Hassan Isihaka ameomba radhi kwa kitendo alichomfanyia Kocha wake, Jackson Mayanja.
Isihaka alimjibu kocha wake ‘mbovu’ wakati alipotaka kumpanga katika mechi dhidi ya Singida United wakati alimtupa jukwaani katika mechi dhidi ya Yanga.
Uongozi wa Simba, jana ulitangaza kumfungia kwa muda usiojulikana na kutokana na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu.
Lakini leo, Isihaka ameuomba uongozi wa Simba kumsamahe.
“Kama binadamu nimekosea, halikuwa lengo langu. Ninachoomba nisamehewe kama mmoja wa wachezaji na vijana wa Simba,” alisema Isihaka.
Wadau wengi wa soka, wameonekana kufurahishwa na kitendo cha Isihaka kuamua kuomba radhi.







0 COMMENTS:
Post a Comment