Kipa wa Simba, Peter Manyika amesema walizungumza na nahodha wao Hassan Isihaka akutane na kocha wake, Jackson Mayanja na kumuomba radhi.,
Manyika amesema yeye na wenzake walifanya hivyo, kwa kuwa suala la kufungiwa linaumiza na wao wasingependa kumkosa Isihaka.
“Sisi ni binadamu na kila mtu anaweza kukosea, kwa kuwa jambo limetokea tumezungumza na Isihaka naye amekubali kweli ni kosa.
“Hivyo tumemwambia aombe radhi, naye amekubaliana na hilo. Kweli amekosea lakini tumsamehe,” alisema Manyika ambaye ni rafiki mkubwa wa Isihaka.
Manyika na Isihaka, walikuwa vijana waliocheza kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Simba Oktoba, 2014.







0 COMMENTS:
Post a Comment