KHANFI |
Baada ya kufichaficha, hatimaye APR ya Rwanda
imetangaza kuingia mkataba kimyakimya na Kocha Mtunisia, kocha Nizar Khanfi.
Kocha huyo aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Tunisia,
anatarajia kutua nchini Rwanda Jumapili na Jumatatu, ataanza kazi huku mechi yake ya kwanza ya kimataifa itakuwa dhidi ya Yanga.
Uongozi wa APR inayomilikiwa na jeshi umatangaza kumpa
kocha huyo miezi sita ili kuona kama inaweza ikampa mkataba wa muda mrefu.
APR inajiandaa kuivaa Yanga wiki ijayo kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali.
0 COMMENTS:
Post a Comment