March 23, 2016

TAMBWE NA KIIZA
Kocha wa Simba SC, Mganda, Jackson Mayanja, hataki kusikia suala la kwamba mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe anatwaa kiatu cha ufungaji bora mbele ya straika wake, Mganda, Hamis Kiiza.

Mayanja amesema anashangaa watu wanavyopiga mahesabu kuwa Kiiza anaweza kupitwa na Tambwe kwa kufunga mabao mengi zaidi na mwisho kuondoka na kiatu hicho kisa kikiwa ni Tambwe kucheza mechi chache mpaka sasa dhidi ya Kiiza kwenye Ligi Kuu Bara.

Mpaka sasa mchuano wa kutwaa kiatu hicho unaonekana kuwa mkali baada ya kinara Kiiza kufunga mabao 19 baada ya mechi 24, akifuatiwa kwa karibu na Tambwe aliyefunga 17 katika mechi 21 pekee za Yanga.

MAYANJA NA KIIZA

Mayanja amefunguka kuwa yeye haamini katika viporo ilivyonavyo Yanga kama Tambwe anaweza kufunga mabao mengi na kumfikia mshambuliaji wake kwa kuwa hakuna anayejua ndani ya dakika 90 nini kitatokea, zaidi anaamini Kiiza ndiye atakayenyakua tuzo hiyo.

“Tambwe siyo Mungu wa soka, ushindani ni mkali lakini huwezi kusema kwamba ni lazima Tambwe ampite Kiiza kwa kuwa yeye ana mechi tatu bado hajacheza. Hakuna anayejua nini kitatokea katika michezo hiyo, kwa hiyo ni bora kusubiri matokeo kuliko kumpa mtu nafasi mapema.

“Ningependa kuona Kiiza anachukua hiyo tuzo, amejitahidi sana kufunga. Kwa hiyo kama akitwaa itakuwa safi,” alisema Mayanja aliyeiongoza Simba kushinda michezo 10 kati ya 11 ya ligi kuu mpaka sasa.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV