Mshambuliaji wa Norwich ya England, Dieumerci Mbokani, ni kati ya watu walionusurika kuwawa katika shambulio la kigaidi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Brussels Airport.
Mbokani alikuwa njiani kwenda kujiunga na timu yake ya taiga ya DR Congo iliyo na majukumu ya kitaifa. Mashambulizi ya kigaidi jijini Brussels yameua watu 34.
Ingawa hakuumia, lakini straika huyo alipata mshituko na inaelezwa alirejeshwa kwenda kujiunga na familia yake ingawa yeye alikuwa tayari kuendelea na safari kwenda DR Congo.
Wanamichezo mbalimbali wakiwemo wanasoka wamekuwa wakiombeleza kuonyesha kutofurahishwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mjini Brussels nchini Ubelgiji.
Wanamichezo hao wakiwemo wanasoka wanaocheza katika ligi kubwa za soka barani Ulaya kama England, Italia, Ujerumani wameelza masikitiko yao kupitia mitandao ya Twiter, Facebook na Instagram wakisisitiza ulinzi unapaswa kuimarishwa barani Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment