Kama unakumbuka, Coastal Union ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kuzifunga timu vigogo msimu huu, sasa kocha wa kikosi hicho, Ally Jangalu ameapa kushinda dhidi ya mahasimu wao African Sports leo Jumamosi.
Coastal Union imeifunga Yanga (mabao 2-0), Azam FC bao 1-0 na Simba katika Kombe la FA mabao 2-1, lakini katika Ligi Kuu Bara ipo mkiani na pointi 22 wakati African Sports ina pointi 23 juu yao.
Jangalu amesema: “Najua utakuwa mchezo mgumu, kama unavyojua bado timu yetu haipo salama tutapambana kubaki ligi kuu kwa kushinda mechi hii.”
Timu zote tatu za mkoa wa Tanga, yaani African Sports, Coastal na Mgambo Shooting zinapambana kuokoa 'roho' zao kuepuka kuteremka daraja.
Wa kufungwa tu nyie ili mwakani tusiwaone
ReplyDelete