April 30, 2016


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana kesho kupitia kesi za washambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, lakini klabu hiyo imesema haitakubali endapo wachezaji hao watafungiwa.

Si unajua sifa za Shirika la Upelelezi la Marekani la FBI linavyojulikana kwa kuzima hujuma kibao dhidi ya taifa hilo kubwa, sasa Baraza la Wazee wa Yanga limesema limeshtukia hujuma zilizopangwa kuwavurugia mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kwa mujibu wa TFF, wachezaji hao na wengine 13 wenye kesi katika mashauri yaliyowasilishwa dhidi yao, watajadiliwa siku hiyo.

Kamati hiyo, itapitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa juu ya wachezaji na viongozi wa klabu mbalimbali, baadhi yao wakiwa ni Shomari Kapombe, Aishi Manula na Kocha wa Azam FC, Stewart Hall na daktari wa Coastal Union, Mganga Kitambi.

Ngoma anatuhumiwa kwa kosa la kumpiga kichwa Hassan Kessy wa Simba na Tambwe anashutumiwa kumshika sehemu za siri Juuko Murshid pia wa Simba.

Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Hashimu Mwika, alisema kwa taarifa walizozipata TFF, kamati hiyo imepanga kukutana kwa nia moja pekee ya kuwafungia Ngoma na Tambwe.

“TFF wakimwaga mboga sisi tutamwaga ugali, kuna taarifa za chinichini kuwa kamati ya nidhamu imepanga kuwafungia Ngoma na Tambwe, hizi ni njama za kutupunguza makali.


“Hatutakubali katika hili, kwa sababu mwanzoni wakati ratiba inatolewa ya ligi kuu, walipanga mechi zote tano za mfululizo tumalizie mikoani tukakaa kimya, walivyoona timu yetu inafanya vizuri wameona wapange njama za kuwafungia wachezaji wetu Ngoma na Tambwe,” alisema Mwika.

1 COMMENTS:

  1. Haya sasa,tunaimbiwa TFF ni ya YANGA hapo ikoje?Hii kesi ya muda mrefu sana,kwa nini haikufanyika siku zote ije ifanyike muda huu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic