April 10, 2016

MANARA

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara amepata ajali mbaya.

Manara amepata ajali baada ya kuchomoka tokea ndani ya Bajaj na kuanguka barabarani.

Kuanguka huko kumesababisha Manara kupata majeraha sehemu za mkononi na usoni hukua kisema amenusurika kifo kutokana na ajali hiyo.

Manara ameelezea tukio hilo:

“Nilikuwa nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj. Sasa tukio hilo limetokea hivi; Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa sijashika, ndiyo nikachomoka.

“Hakika nimeumia na nina maumivu makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.”


SALEHJEMBE INATOA POLE KWA MANARA NA KUMUOMBEA APATE NAFUU MAPEMA NA KUPONA KABISA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV