April 29, 2016

PATRICK KLUIVERT AKIWA NA JUSTINE KLUIVERT

Mtoto wa nyota wa zamani wa Ajax, Patrick Kluivert amesaini mkataba wa kwanza wa kucheza soka la kulipwa.

Justin Kluivert ,16, amesaini mkataba wake wa kwanza wa soma la kulipwa katika klabu ya Ajax ambayo baba yake alichipukia.

Ingawa haijaelezwa kinda huyo amesaini mkataba wa muda gani baada ya baba yake kutupia kwenye instagram, lakini anaonekana kwenda kukamilisha ndoto yake kwa kuwa alijiunga na Ajax tokea akiwa na umri wa miaka 6.

Ameichezea timu ya watoto kwa miaka 10 na sasa anajiunga na timu vijana huku akiwa anapewa nafasi ya kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kabisa hapo baadaye.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV