April 30, 2016

KIUNGO wa Simba, Mwinyi Kazimoto, leo anatarajiwa kufunga ndoa na mchumba wake aliyefahamika kwa jina moja la Regina, hivyo hataichezea timu yake dhidi ya Azam FC.


Simba na Azam kesho Jumapili zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, ambayo itatoa njia ya bingwa au timu itakayoshika nafasi ya pili.

Kazimoto anatarajiwa kufunga ndoa leo hii katika kanisa moja lililopo Kongowe nje kidogo ya Dar es Salaam, hivyo hataweza kucheza mechi hiyo.

Kwa upande wake Ibrahim Ajib, yeye ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano alizopata katika mechi zilizopita za timu hiyo.


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kwake lakini amejipanga kuhakikisha anashinda mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic