May 21, 2016


Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, amesema msimu huu amelazimika kuwa na lundo la wachezaji wakongwe kwani aliipokea timu hiyo katikati ya msimu, lakini msimu ujao anataka ‘mafaza’ wasiozidi watatu tu.

Phiri, raia wa Malawi, amesema anataka kujaza wachezaji vijana kikosini mwake msimu ujao akiamini wanaweza kumletea mafanikio.

Kocha huyo wa zamani wa Free States ya Afrika Kusini, amekwenda mbali kwa kusema anataka robo tatu ya kikosi kizima kiwe ni vijana, tofauti na sasa ilivyo na wakongwe hawatazidi watatu.

Mbeya City inayoshika nafasi ya nane katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 34, ina wakongwe kama Juma Kaseja, Them Felix, Hassan Mwasapili, Anthony Kalyesubira, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Haruna Moshi ‘Boban’ na Steven Mazanda.

“Msimu huu nimekuta timu imeshasajili, lakini msimu ujao lazima nisimamie falsafa yangu. Ninataka robo tatu ya kikosi changu kiwe na wachezaji vijana. 

“Nitabaki na wakongwe watatu tu, ila siwezi kuwataja sasa kwa kuwa ligi bado inaendelea, nataka kuwatumia vijana kwani naamini nitafanikiwa nao,” alisema Phiri.

Wakati Phiri akisema hayo, taarifa zinasema Mbeya City ipo katika harakati za kumsajili straika wa Ndanda FC, Atupele Green. Mbeya City kesho Jumapili inamaliza ligi kuu kwa kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

SOURCE: CHAMPIONI



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic