MUSOTI (KUSHOTO)... |
Klabu ya Simba imelipa deni lililokuwa ikidaiwa na beki Mkenya, Donald Mosoti.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) liliiagiza Simba kuwa imelipa deni hilo hadi mwisho wa mwezi huu baada ya kutoa siku 30 au Simba iteremshwe daraja.
HANS POPPE |
Fedha hizo zilikuwa ni jumla ya Sh milioni 70 pamoja na faini mbalimbali.
Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema jana kwamba walishalipa.
“Tulishalipa deni hilo, kila kitu kinakwenda vizuri. Wala hakukuwa na sababu ya kutangaza,” alisema kiongozi huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment