May 25, 2016


Yanga imeitwanga Azam FC kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kubeba Kombe la Shirikisho.

Ushindi huo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, unaifanya Yanga kuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Ilikuwa mechi ya kuvutia huku Amissi Tambwe akifunga mabao mawili na moja likikwamishwa kimiani na Deus Kaseke.

Bao pekee la Azam FC lilifungwa na Didier Kavumbagu aliyeingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya nahodha John Bocco. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV