May 16, 2016


Straika wa Simba, Ibrahim Ajib aliyepo nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, amesema anaendelea vizuri na ana asilimia kubwa za kufaulu majaribio hayo.

Ajib ambaye alitimkia nchini humo Jumatatu ya wiki iliyopita, anaendelea kufanya majaribio kwenye kikosi cha Golden Arrows kinachoshiriki Ligi Kuu ya Sauz na mpaka sasa tayari ameshafanya kwa siku tatu mfululizo na kikosi hicho kabla ya kupumzika jana na kuendelea tena leo.

“Nashukuru Mungu kwa siku ya kwanza niliyofanya mazoezi kocha ameonyesha kunikubali, mpaka sasa nimeshafanya mazoezi kwa siku tatu na leo (jana) tumepumzika ila kesho (leo) kama kawaida,” alisema Ajib.

Awali meneja wake, Juma Ndambile alisema kama atashindwa katika timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, atakwenda kufanya majaribio Amazulu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Afrika Kusini.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV