May 6, 2016





Kilichobaki kati ya Yanga na beki Hassan Kessy ni kuweka saini kwenye mkataba pekee.

Yanga na beki huyo ambaye mkataba wake Simba unakwisha, wamefikia mwafaka baada ya kukubaliana kila kitu na leo matarajio makubwa atasaini rasmi na kuwa mchezaji wa Yanga.

Si unakumbuka Kessy aliomba apewe jezi namba 25 iliyokuwa inavaliwa na Emmanuel Okwi. Sasa huenda akakabidhiwa leo rasmi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimesema baada ya kuona hana uhakika wa kubaki Msimbazi, Kessy amefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na wamemalizana kwa kuwa mkataba wake Simba, ‘umeisha’.

“Nakuambia kila kitu kati ya Yanga na Kessy kimeisha. Suala la kusaini ndiyo lilikuwa halijakamilika, ila Ijumaa, mambo yote yanakamilika na Kessy anasaini kuanza kuichezea Yanga,” kilieleza chanzo.

Kessy amekiri kufanya mazungumza na Yanga pia.

“Kweli lakini nafikiri meneja wangu ndiye anaweza kulizungumzia hilo,” alisema.

Alipotafutwa meneja wake, Tippo Athumani ‘Zizzou’ ambaye ni kiungo wa zamani wa Milambo ya Tabora na Coastal Union, pia alikubali.


“Kweli tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Lakini vizuri tukimaliza, tunaweza kuwaeleza kila kitu,” alisema Tippo.

5 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Hahahahahaha!unanikumbusha ya nyani,
      "SIZITAKI MBICHI HIZI"

      Delete
  2. KESSY MZURI SANA NA HASA AKIPATA KOCHA KAMA HANS VAN DER PLUIJN.
    PLUIJN ANAWEZA KUMSOMA MTU NA KUMBADILISHA,TUKUMBUKE NGOMA ALIVYOKUWA WAKATI ANATUA YANGA.HONGERA KESSY,KUSEMA KWELI WATU WANALILIA KUCHEZEA YANGA NA AZAM SASA HIVI.KWA WA MCHANGANI FIGISUFIGISU NYINGI SANA LABDA KAMA WATABADILISHA UONGOZI

    ReplyDelete
  3. Naamini sasa hahitaji kutafutia sababu ya kumpa pasi Ngoma ili Yanga ishinde, au kucheza rafu mbaya ili apewe kadi nyekundu atoke.

    ReplyDelete
  4. Inaelekea mna publish tu comment ambazo zina mulekeo / mlengo mnaoupenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic