May 15, 2016


Kikosi timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, cha Serengeti Boys kimefanikiwa kuanza michuano ya vijana ya nchini India kwa sare ya bao 1-1.

Serengeti Boys ambayo ilionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza, ilifika mapumziko ikiwa na sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa shuhuda, mechi hiyo ilikuwa ngumu kipindi cha pili mwanzoni. Lakini kipindi cha pili mwishoni Serengeti Boys wakashambulia zaidi ingawa hawakufanikiwa kufunga.

Mechi inayofuata ni Alhamisi ijayo na Serengeti Boys watashuka uwanjani kuwavaa Korea Kusini katika mechi yao ya pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV