May 21, 2016


Straika wa Mwadui FC, Jerry Tegete, amelishukia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akidai hajui hatma ya malipo ya fedha anazoidai Yanga baada ya malalamiko yake kufika kwenye shirikisho hilo.

Tegete anaidai Yanga Sh milioni 10, ikiwa ni malipo yake ya kuvunjiwa mkataba msimu wa 2014/2015 kabla ya kutimkia Mwadui.

Tegete alisema suala lipo mezani kwa Kamati ya Nidhamu ya TFF iliyokutana Julai 3, 2016 na kujadili masuala mbalimbali likiwemo la Geita Gold, lakini anashangaa limewekwa pembeni na kutojadiliwa.

Tegete alisema, mara baada ya suala lake kutojadiliwa, alimtafuta Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Uanachama wa TFF, Eliud Peter Mvela lakini hakumpa majibu sahihi juu ya madai yake.  

“Ninavyosikia Yanga kwa kushirikiana na mmoja wa viongozi wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, wamepanga kutudhulumu mimi na wengine tunaowadai, kiukweli sitakubali kuona haki yangu inapotea.

“Yanga tayari wamenilipa Sh milioni 10 na imebakia Sh milioni 10 baada ya kuvunja mkataba wangu wa mwaka mmoja uliobaki kuichezea Yanga, naomba Malinzi (Rais wa TFF, Jamal) anisaidie nilipwe,” alisema Tegete.

Alipotafutwa Mvela kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi haikupatikana, lakini Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa akizungumzia suala hilo alisema: “Ngumu kulizungumzia hilo, kwani halipo kwenye meza yangu.”

Sh Mil 20
Jumla ya fedha 

za madai ya Tegete kwa Yanga

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic