May 20, 2016


Mabingwa wa Tanzania, Yanga ambao kikosi chao kimewatoa kimasomaso Watanzania kwa kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, wamerejea nchini.

Yanga wamerejea nchini na kupokelewa na mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).


Ilikuwa furaha kuu, haikuishia hapo, wakaanza safari ya kukatisha mitaa huku mashabiki wakikimbia barabarani.

Mashabiki hao waliandamana kupitia barabara ya Pugu hadi walipofika katika jengo la Quality Plaza zilizopo ofisi za Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

Mashabiki wengine walikuwa wamepanda juu ya miti na juu ya majengo mbalimbali, lengo likiwa ni kutaka kuwaona Yanga.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV