June 15, 2016



Klabu ya Azam FC imezidi kushikilia msimamo wake wa kutaka kumuingiza kundini, kiungo mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Mkopi kwa lengo la kumuongezea nguvu nahodha msaidizi, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’, hata hivyo makubaliano yao yamegota kwenye kipengele cha masilahi.

Kiungo huyo ambaye msimu uliopita alifanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Mwezi Februari, amekuwa tegemeo la Prisons na kuiwezesha kumaliza katika nafasi ya nne huku yeye akimaliza akiwa na mabao saba.

Chanzo cha habari kutoka kwa nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, kimesema kuwa ugumu umekuja kwenye kiwango cha fedha za usajili.

Imeelezwa kuwa uongozi wa Azam umekwenda na milioni 15, lakini mchezaji mwenyewe anataka kati ya milioni 25 hadi 30.

Mbali na nafasi ya Sure Boy, pia Mkopi ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji.

“Mazungumzo bado yapo na kikubwa ni maslahi. Azam wanataka kumpa milioni 15 lakini amegoma anataka milioni 30, ama ikipungua basi milioni 25. Ishu ya mshahara makubaliano ya awali ni milioni moja lakini hilo litakuja baada ya makubaliano kwenye fedha za usajili,” kilisema chanzo chetu.


Alipotafutwa Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, alishindwa kukanusha wala kukubali taarifa hizo, zaidi aliishia kusema kila kitu kitawekwa hadharani Julai Mosi, 2016.

SOURCE; CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic