June 15, 2016RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA


Klabu ya Simba imeamua kuongeza kasi zaidi katika suala la kupata kocha mpya.

Simba imeamua kufanya hivyo baada ya juhudi zake za kumnasa Kalisto Pasuwa kugonga mwamba maana amekubali kubaki na timu yake ya taifa ya Zimbabwe ambayo ameiwezesha kufuzu Afcon.

“Tunaona suala la kocha liwe namba moja. Wachezaji tayari tumeanza kusajili vizuri tu,” kilisema chanzo cha uhakika.

“Lakini ni vizuri kuangalia kuhusiana na kocha maana yeye anatakiwa kuja mapema na kuanza na kikosi.

“Kweli juhudi zinaendelea kwa nguvu kabisa. Lakini ni suala la kusubiri uhakika pia makubaliano,” kiliongeza chanzo.


Taarifa nyingine zimesema, kama watachelewa kupata kocha, bado Kocha Msaidizi na kaimu kocha mkuu, Jackson Mayanja ataianza kazi hiyo ya maandalizi wa mwanzo wa msimu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV